Mji wa Belem nchini Brazil ni mwenyeji wa mkutano wa kilele wa msitu wa Amazon ambapo watunga sera na maafisa wengine wanakutana kujadili jinsi ya kukabiliana na changamoto kubwa za kulinda chanzo muhimu cha mazingira.
Matangazo
Msitu wa mvua wa Amazon una ukubwa wa mara mbili wa nchi ya India na unapatikana katika nchi nane. Ni msitu muhimu kwa kunyonya gesi chafu ya kaboni, una asilimia 20 ya hifadhi za maji safi duniani na una takriban spishi 16,000 za miti.
Ila serikali zimeuchukulia msitu huu kama eneo la kukoloniwa na kutumika vibaya pasi na kuzingatia haki za watu asili wanaoishi katika msitu huu. Lakini kipi ni kitisho kikubwa cha kimazingira kwa msitu wa Amazon?
Kilicho juu kwenye orodha ya vitisho hivyo ni ukataji wa miti. Msitu wa Amazon umepoteza zaidi ya ekari milioni 211 au asilimia 13 ya eneo lake la asili. Sehemu kubwa ya uharibifu huo umefanyika katika nusu karne iliyopita huku Brazil, ambayo ni mwenyeji wa thuluthi mbili ya msitu huo, ikiwa sehemu iliyoshuhudia uharibifu mkubwa.
Hakuna sehemu iliyo na uharibifu mkubwa zaidi kuliko jimbo la Para ambalo mji wake mkuu ni Belem. Asilimia 41 ya ukataji miti katika msitu wa Amazon Brazil umefanyika katika jimbo la Para, ambako sehemu kubwa ya ardhi imebatilishwa na kufanywa eneo la kufuga ng'ombe milioni 27. Kulingana na mtandao mmoja wa makundi ya kimazingira, hili ndilo eneo linaloongoza kwa utoaji wa gesi chafu katika majimbo ya Brazil.
Kitisho chengine cha mazingira ni mabwawa makubwa ya kufua umeme hasa nchini Brazil, uchimbaji madini na mafuta huku mambo hayo yakiwa na athari kwa maji na kuyatatiza maisha ya watu wa asili.
Kutoekeza kikamilifu katika miundo mbinu ni jambo linalomaanisha kwamba sehemu kubwa ya maji machafu kutoka majumba yaliyoko katika msitu huo wa mvua, yanaingia moja kwa moja kwenye njia za maji. Msitu wa Amazon katika miaka ya hivi karibuni pia umeshuhudia mafuriko na ukame.Amazon, makampuni makubwa yaahidi kuajiri maelfu ya wakimbizi
Mambo mengine ambayo ni kitisho kwa msitu huu ni ujenzi wa barabara na uhalifu. Awali serikali katika maeneo hayo zilikuwa zikitengeza barabara katika msitu huo kwa kukata miti tu ila mvua zimekuwa ziharibu barabara hizo. Kutokana na hilo, ikachukuliwa hatua ya kuzitia lami ili iwe rahisi pia kwa usafirishaji wa bidhaa za kilimo.
Hili ni jambo zuri ila liliwasaidia wavunjaji sheria kufika maeneo ya ndani kabisa ya msitu huu na kukata miti kwa ajili ya ufugaji miongoni mwa mambo mengine.
Chengine kilichochangia kwa mashirika ya kihalifu kukita mizizi msituni humo ni ufisadi na kulemaa katika masuala ya utekelezaji wa sheria. Maeneo machache ya mpakani yana ulinzi mkali wa polisi na kumekuwa ushirikiano mdogo wa kimataifa, wakati ambapo magenge ya wahalifu yanashindana kwa njia za ulanguzi wa madawa ya kulevya.
Lakini msitu wa Amazon ni muhimu kwa kiasi gani katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi? Athari za mabadiliko ya tabia nchi hua mbaya zaidi pale mimea ya kuinyonya gesi chafu ya kaboni inapopotea na msitu wa Amazon una umuhimu mkubwa katika kunyonya gesi hii ya kaboni.
Hazina za kiasili zilizo katika hatari ya kupotea
Kutoka msitu wa Amazon hadi bahari ya Dead Sea, mandhari mengi ya kiasili yenye mvuto wa aina yake yako hatarini kutoweka kutokana na utalii na athari ya mabadiliko ya tabia nchi.
Picha: picture-alliance/JOKER/W. G. Allgöwer
Msitu wa Amazon: Mapafu ya Ulimwengu
Msitu huu umeenea katika nchi tisa katika eneo la Marekani ya Kusini, na ni muhimu kwa mazingira kwani kando na kudhibiti viwango vya gesi chafu hewani, hhuhifadhi wanyama pori na mimea tofauti. Viwango vya ukataji misitu vilikuwa juu mnamo mwaka 2020, huku miti ya kiasili ikikatwa ili kupata nafasi ya ufugaji, ukulima na uchimbani madini. Kutokana na ukataji wa misitu, viwango vya mvua vimeshuka.
Picha: picture-alliance/dpa/M. Arrevad
Mwamba Mkuu wa Matumbawe: Miaka 80 imebaki
Aina 400 za matumbawe, aina 500 ya samaki na viumbe wengine wa baharini kama kasa wanaishi katika eneo hili la Great Barrier Reef karibu na pwani ya kaskazini mashariki mwa Australia. Lakini kutokana na viwango vya juu vya joto, nusu ya mwamba huo tayari umepotea.
Picha: University of Exeter/Tim Gordon
Darwin: Viumbe vilivyoko hatarini kupotea
Visiwa vya Galapagos vya Ecuador, vilivyoko kilomita 1000 kutoka pwani ya Magharibi mwa Marekani ya Kusini ni turathi na kumbukumbu za dunia kwani wanyama na mimea mbalimbali vimefanya visiwa hivyo kuwa maskani yao. Eneo hilo la kiasili linakabiliwa na kitisho kutokana na uvamizi, uchafuzi wa mazingira, utalii na uvuvi uliopitiliza.
Picha: imago/Westend61
Himalayas: Milima ya barafu yenye kuyeyuka
Mwaka 1980, mtafiti Reinhold Messner alifanikiwa kupanda mlima wa Everest bila ya msaada wa vifaa vya Oksijeni. Imepita miongo kadhaa sasa tangu mlima mrefu zaidi duniani kupandwa zaidi ya mara 10,000 Viwango vya barafu katika milima ya Himalayas vinapungua na barafu inaendelea kuyeyuka kutokana na ongezeko la joto duniani.
Picha: AFP/Project Possible
Hifadhi ya kitaifa ya miti ya Josua
Mwisho wa Karne, miti ya Josua, ambayo hifadhi ya kitaifa ya Carlifonia inatumia jina hilo, huenda ingepotea kabisa kwa sababu ya ongezeko la joto duniani. Miche ya mimea ya jangwa inakabaliwa na hatari ya kutoota kutokana na ongezeko la ukame. Na licha ya kuwepo misimu ya baridi, miti hiyo ya jangwa bado inatoa maua machache mno. Pia, ukuaji wa nyasi kunaongeza hatari ya eneo hilo kuchomeka.
Picha: picture-alliance/United-Archives
Hakuna theluji Kilimanjaro
Mlima mkubwa zaidi barani Afrika wenye "koni" tatu za Volcano ambayo ya juu zaidi imepewa jina la Kibo una urefu wa mita 5895 juu ya usawa wa bahari. Kilele chake kimepoteza takriban asilimia 85 ya theluji kati ya mwaka 1912 na 2019. Watafiti wanashuku kuwa, kupungua kwa theluji kwenye mlima Kilimanjaro kumesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
Picha: picture-alliance/AP Photo
Machu Picchu: Alama ya mazingira ya Utalii
Zaidi ya watalii milioni 1.5 kila mwaka hutembelea eneo hili la kihistoria la Incan Citadel nchini Peru. Shirika la umoja wa mataifa la UNESCO linapendekeza wageni wachache kuzuru eneo hilo, likitoa sababu kuwa idadi kubwa ya watalii kutalifanya eneo hilo kuwa dhaifu. Watalii hao pia wanatajwa kuwa na athari hasi kwa mazingira ya eneo hilo.
Picha: picture-alliance/C. Wojtkowski
Maldives: Kutoweka baharini
Hakuna njia nyengine ya usafiri iliyo na athari hasi kwa mazingira kama usafiri wa ndege. Wakati viwango vya joto duniani vinazidi kuongezeka, viwango vya maji ya bahari pia vinazidi kupanda hadi sentimita 3.7 kwa mwaka. Kutokana na kuwa Maldives iko mita 1.5 juu ya usawa wa bahari, kuna hofu kuwa kupanda kwa maji ya bahari kuna hatarisha uwepo wa visiwa vya Maldives.
Picha: DW/R. Richter
Ziwa Nicaragua: Mwisho wa utulivu na mandhari mazuri?
Katika siku zijazo, meli kubwa za kubeba mizigo huenda zikatumia ziwa kubwa katika eneo la Marekani ya kati badala ya boti dogo kama sehemu ya kuunganisha bahari ya Carribean na bahari ya Pasifiki ili kurahisisha usafiri. Wanamazingira wana wasiwasi kuwa hali hiyo huenda ikaathiri mfumo wa maisha katika ziwa hilo la maji baridi, ambalo linahifadhi wanyama mbalimbali kama vile papa
Picha: picture-alliance/AP
Kifo cha ziwa la Chumvi-Dead Sea
Ziwa hili la bara Asia liko mita 420 chini ya usawa wa bahari. Dead Sea ndio ziwa la pekee duniani lililoko chini ya ardhi. Hata hivyo, ziwa hili linaendelea kukauka maji kila uchao. Hali ya kuzuia usambaji wa maji kutoka mto Jordan na Israel katika ziwa hili imesababisha viwango vya maji kuendelea kushuka kwa takriban mita moja kila mwaka.
Picha: picture-alliance/JOKER/W. G. Allgöwer
Picha 101 | 10
Mwanakemia Luciana Gatti, aliyekuwa mwandishi mwenza katika jarida la Asili, lililobaini kuwa eneo la mashariki la msitu wa Amazon lililoshuhudia ukataji mkubwa wa miti, kwa sasa hivi halifyonzi tena gesi ya kaboni na badala yake ni chanzo cha gesi hiyo. Gatti anasema nusu ya eneo la Amazon mashariki lililokatwa miti linastahili kupandwa miti hiyo, ili msitu huo wa mvua uendelee kusalia kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.
Ila maendeleo yanaweza kufanyika katika msitu huu wa Amazon bila uharibifu wa mazingira? Marcelo Salazar, mkongwe wa kazi za ushauri na mazingira anasema, msitu huu ni mkubwa mno na unakanganya kiasi cha kwamba hakuna suluhu moja la maendeleo katika maeneo tofauti.
Salazar anasema kwanza serikali zinastahili kutoa haki za kiafya, kielimu na ulinzi wa ardhi ili uchumi wa msitu huo uweze kufanya kazi kikamilifu. Chengine anachopendekeza Salazar ni, kueleimishwa kwa watu wa asili kwenye msitu huo kuhusiana na jinsi ya kuwasilisha changamoto za msitu huo kwa ajili ya kuwasaidia walioko nje kuuelewa na pia kuwavutia wawekezaji.