1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUfaransa

Mkutano wa kilele wa Paris kujadili ufadhili wa kimataifa

19 Juni 2023

Viongozi wa mataifa mbalimbali duniani watakutana wiki hii mjini Paris kwa lengo la kufikiria upya ufadhili wa kimataifa katika zama hizi mpya zinazogubikwa na mabadiliko ya hali ya hewa

Frankreich, Paris | Präsident Macron TV-Ansprache zur Rentenreform
Picha: Sarah Meyssonnier/REUTERS

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema mkutano huo wa Kilele wa Mkataba Mpya wa Kifedha wa Kimataifa utakaoanza siku ya Alhamisi, unalenga kujenga "makubaliano mapya" ili kufikia malengo jumla kukabiliana na umaskini, kuzuia ongezeko la joto duniani na kulinda bayoanuai.

Miongoni mwa mambo mengine, viongozi hao kutoka mataifa zaidi ya 50 akiwemo Rais wa Kenya William Ruto na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo, pamoja na Waziri Mkuu wa Barbados Mia Mottley, watajadili kuhusu mtazamo mpya wa kimuundo wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia.

AFP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW