1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Kilele wa SADC Kinshasa

17 Agosti 2022

Kunafanyika mkutano (17.08.2022) mjini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mkutano wa kikele wa 42 wa maraïs pamoja na viongozi wa serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Malawi Präsident Lazarus Chakwera
Picha: AMOS GUMULIRA/AFP

Mkutano huo unaoshirikisha nchi kumi kati ya kumi na sita zinazounda jumuiya hiyo ulikuwa na mada kukuza uchumi wa viwanda kupitia usindikaji wa mazao ya kilimo, maendeleo ya madini na uendelezaji wa thamani  ili kufikia uchumi jumuishi na endelevu.

Hio ni mada muhimu sana ambayo washiriki katika kazi za Mkutano huo wa 42 wa marais pamoja na viongozi wa Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika wameifikiria. Lakini cha muhimu ni kuona SADC kujihusisha na suala la kuurejesha usalama mashariki mwa Kongo. Ndivyo alivyoeleza Christian Longange, mmoja wa wafalme wa maeneo ya Mwenga mkoani Kivu kusini.

Mwakilishi wa Mwenga amesema vita inawatesa sana.

Walinza amani wa Afrika, MsumbijiPicha: Simon Wohlfahrt/AFP/Getty Images

Zaidi alisema "Sisi tumekuwa wahanga wa vita. Tangu vita vyote vilivyoanza watu wanakufa na kunakuwa na wasiwasi katika vijiji vyetu. Na sisi kama viongozi wa asili wa Waluzimu katika maeno ya Mwenga, tunaomba mkutano huu uwe anafanyika mara kwa mara kwa kuleta amani katika Kivu kusini na Kivu kaskazini.. Wakati maraïs wote wanakutana hivyo watatafuta suluhisho."  

Miongoni mwa mambo muhimu yaliyogubika mkutano huo ni pamoja na makabidhiano ya uenyekiti wa SADC kutoka kwa Rais aliyemaliza muda wake, Lazarus Chakwera wa Malawi, kwenda kwa Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mkutano huo unafanyika hivi huku Kongo ikikabiliana na waasi wa M23 katika eneo lake la mashariki. Kongo imeishutumu Rwanda kuwaunga mkono waasi hao. Nimemuuliza Vincent Magwenya, msemaji wa raïs Cyrille Ramaphosa wa Afrika kusini, kama kuna bahati Sadc kusaidia kutatua mgogoro mashariki mwa Kongo.

Raïs Ramaphosa alikuwa akiongoza timu ya Sadc kwa kushiriki katika utatuzi wa migogoro ya kisiasa pamoja na uhusiano kuhusu usalama. Alipotowa ripoti yake hapo jana aligusia ujumbe wa Sadc huko Musumbiji, upatanishi wake huko Lesotho na pia kagusia swali la waasi wa M23.

Soma zaidi:Burundi yatuma vikosi vyake mashariki mwa DRC

Hapo awali mkutano ulikuwa umepangwa hadi Alhamisi, lakini kazi zitafungwa leo Jumatano kufuatia ratiba zilizojaa shughuli nyingi za maraïs wa Nchi mbalimbali.

Nchi kumi ndizo ziwakilishwa na marais wao, nazi ni Tanzania,  Shelisheli, Namibia, Malawi, Afrika Kusini, Msumbiji, Zimbabwe,  Zambia, Mauritius na Eswatini.

DW: Kinshasa.