Mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika wamalizika Kampala
27 Julai 2010Umoja wa Afrika umeidhinisha ombi lililotolewa na Jumuiya ya IGAD, la kutuma majeshi zaidi nchini Somalia. Hatua hiyo imeidhinishwa rasmi leo mjini Kampala Uganda, ambako Mkutano wa viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika umemalizika leo. na kwamba hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni wiki chache tu baada ya waasi wa Somalia wa al Shaabab, kufanya shambulio la bomu katika mji huo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 70.
Djibouti na Guinea zimeahidi kutuma majeshi yao Somalia kusaidiana na yale ya Burundi na Uganda ambayo yanalinda usalama nchini humo, chini ya Umoja wa Afrika.
Wakati hayo yakijiri, kikao cha leo ambacho ni cha mwisho, kimetoa maazimio ya mkutano huu wa Umoja wa Afrika ambao umekuwa ukifanyika, mada ikiwa ni Afya ya wanawake na watoto.
Kutoka Uganda mwandishi wetu Leyla Ndinda ametutumia taarifa zaidi.