Mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya waanza Brussels
23 Machi 2023Matangazo
Kanda hiyo kwa wakati huu inatatizwa mambo mengi ambayo viongozi hao wanapaswa kuyaweka mezani ikiwemo mfumuko wa bei, nishati ghali, uhaba wa wafanyakazi na mapungufu ya uwekezaji.
Katika mkutano huo kunatarajiwa kuwa na msururu wa rasimu za sheria zenye kufanikisha mabadiliko katika sera ya viwanda, ikiwemo magaeuzi katika soko la nishati ya umeme, msukumo wa kufanikisha upatikanaji zaidi wa malighafi na kuhama kutoka katika kuitegema China kama chanzo cha teknolojia ya nishati safi.