1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kilele wa viongozi wa G20.

Abdu Said Mtullya11 Novemba 2010

Mkutano wa viongozi wa nchi za G 20 unaanza leo mjini Seoul huku kukiwa na tofauti kubwa baina ya nchi hizo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Ametahadharisha juu ya uwezekano wa kutokea mgogoro mwingine wa fedha duniani.Picha: AP

SEOUL:

Muda mfupi kabla ya mkutano wa viongozi wa G 20 kuanza rasmi mjini Seoul hakuna dalili za mwafaka juu ya mzozo unaohusu hitilafu katika thamani ya sarafu baina ya nchi tajiri za viwanda na zinazoinukia kiuchumi.Pande hizo pia zinakabiliwa na mzozo unaohusu urari wa biashara.

Mwenyeji wa mkutano Rais Lee Myung Bak wa Korea ya Kusini amesema tofauti za maoni zinaendelea kuwapo .Habari zaidi zinasema pia pana uwezekano wa kutokea mvutano baina ya Marekani iliyolemewa na matatizo ya uchumi na nchi kama Ujerumani na China zinazoongoza katika kuuza bidhaa nje.Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema sera ya fedha ya Marekani inaweza kusababisha mgogoro mwingine wa fedha duniani .

Kwa upande wake rais Obama anazitaka Ujerumani na China zipunguze uuzaji wa bidhaa nje na pia ameitaka China ipandishe thamani ya fedha yake.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewataka viongozi wa nchi tajiri waitekeleze ahadi ya kuuondoa umasikini duniani.Katibu Mkuu Ban pia amezitaka nchi za G 20 zichukue hatua zaidi katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW