1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa kimataifa juu ya Ukraine waanza Jeddah

7 Agosti 2023

Wajumbe kutoka nchi zaidi ya 40, zikiwemo Marekani, Ujerumani na China, wamekutana mjini Jeddah nchini Saudi Arabia ili kujaribu kuutafutia suluhu mzozo wa Ukraine.

Saudi Arabien, Dschidda | Ukraine Gipfeltreffen
Picha: Saudi Press Agency/Handout/REUTERS

Wajumbe hao wamefikia makubaliano ya kuendeleza "mashauriano ya kimataifa" ili kujenga msingi wa pamoja kwa ajili ya amani nchini Ukraine.

Wanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya wamebainisha kuwepo kwa uungwaji mkono mpana wa kuendeleza majadiliano kuhusu misaada ya kibinadamu, usafirishaji wa chakula pamoja na masuala ya nyuklia na mazingira.

Soma: Mazungumzo ya amani kuhusu vita vya Ukraine yafanyika Saudi Arabia

Urusi haikualikwa kuhudhuria mkutano huo, lakini ilikuwa ikipewa taarifa na wajumbe wa Saudi Arabia kuhusu maendeleo ya mazungumzo hayo.

Saudi Arabia, ambayo imeandaa na kuwa mwenyeji wa mkutano huo, imesema lengo ni kutafuta "njia ya kisiasa na kidiplomasia" ya kumaliza vita vya Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW