1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMisri

Mkutano wa kuhusu vita Mashariki ya Kati waanza mjini Cairo

21 Oktoba 2023

Mkutano wa kimataifa ulioitishwa na Misri kujadili njia za kumaliza vita kati ya Israel na kundi la Hamas umefunguliwa leo mjini Cairo chini ya uenyekiti wa rais Abdel Fattah El-Sisi wa nchi hiyo

Rais wa Misri - Abdel Fattah El-Sisi wakati wa maadhimisho ya siku ya mazazi ya mtume Mohammed mjini Cairo, Septemba 27,2023
Rais wa Misri - Abdel Fattah El-SisiPicha: Egyptian President Office/ZUMAPRESS.com/picture alliance

Katika hotuba yake Al-Sisi amesema ameitisha mkutano huo kutafuta makubaliano ya njia za kumaliza hali mbaya ya kiutu kwenye Ukanda wa Gaza na kufufua mchakato wa kusaka amani kwa mzozo kati ya Israel na Wapalestina.

Jordan yasema kuwalazimisha wapalestina kuondoka katika makazi yao ni makosa ya uhalifu wa kivita

Akihutubia mkutano huo Mfalme Abdullah wa Jordan amesema kuwalazimisha wapalestina kuondoka kwenye makaazi yao au kuwafanya kuwa wakimbizi wa ndani yatakuwa makosa ya uhalifu wa kivita.

Soma pia: HRW yaituhumu Magharibi kwa unafiki juu ya Gaza

Mkutano huo wa leo unahudhuriwa na viongozi wengi wa mataifa ya kiarabu na wawakilishi kutoka mataifa kadhaa ya magharibi pamoja na China. Marekani iliyo mshirika muhimu wa Israel haijatuma mwakilishi wake hali inayozusha mashaka kuhusu mafanikio ya mkutano huo wa Cairo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW