Mkutano wa kimataifa wa hali ya hewa mjini Bonn
29 Machi 2009Matangazo
Bonn:
Wajumbe zaidi ya 2000 kutoka zaidi ya nchi 180 wanakutana katika mji wa Ujerumani wa Bonn,kwa duru kadhaa za mazungumzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa.Lengo la mkutano huo wa Umoja wa Mataifa utakaodumu siku kumi ni kujiandaa kwaajili ya mkutano wa hali ya hewa utakaoitishwa mjini Copenhagen nchini Danemark December mwaka huu.Mkutano wa kilele wa Copenhagen umelengwa kufikia makubaliano mepya ya kupunguza hali ya ujoto,itifaki ya Kyoto ya kupunguza moshi wa viwandani ,muda wake utakapomalizika mbnamo mwaka 2012.