1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Mkutano wa Korea-Afrika kuangazia madini na biashara

Saleh Mwanamilongo
2 Juni 2024

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol atakuwa mwenyeji wa mkutano wa Korea na Afrika utakaofanyika Jumamnne mjini Seoul.

Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol
Rais wa Korea Kusini Yoon Suk YeolPicha: JEON HEON-KYUN/Pool/REUTERS

Korea Kusini inauelezea kuwa utalenga kupata uagizaji wa madini muhimu na kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Afrika. Maafisa wa serikali ya mjini Seoul wamesema wajumbe kutoka nchi 48 za Afrika watahudhuria mkutano huo.

Hafla ya marais imepangwa kufanyika Jumanne, na kufuatiwa na mkutano wa kilele wa biashara unaohusisha viongozi wa makampuni ya Korea Kusini na Afrika siku ya Jumatano.

Rais Yoon amesema kuna miradi chungu nzima ambapo Korea na Afrika zinaweza kushirikiana katika nyanja nzima ya miundombinu, ikijumuisha ujenzi wa barabara, reli, viwanja vya ndege na bandari, mifumo mahiri ya jiji, na usafirishaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW