1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Uturuki na Afrika kufanyika wiki ijayo Djibouti

Angela Mdungu
25 Oktoba 2024

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uturuki Akan Fidan, anatarajiwa kuelekea Djibouti wiki ijayo kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa Uturuki na Afrika.

Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan alipotembelea Belgrade, Serbia Septemba 7, 2022.
Rais wa Uturuki Tayyip Erdogan alipotembelea Belgrade, Serbia Septemba 7, 2022.Picha: Marko Djurica/REUTERS

Mawaziri hao watajadili namna ya kuimarisha uhusiano kati ya Ankara na bara la Afrika. Hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Uturuki. Mmoja wa maafisa wa wizara hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina amesema mkutano huo utatathmini mikutano iliyofanyika mwaka 2021 na kujadili zaidi namna ya kuongeza zaidi ushirikiano.Mkutano wa wiki ijayo unatarajiwa kuhudhuriwa na mataifa 14. Uturuki ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO imekuwa ikipambana kuongeza ushawishi wake Afrika katika miaka ya hivi karibuni na kutoa usaidizi wa kijeshi, kidiplomasia na kusaini mikataba katika sekta mbalimbali na baadhi ya nchi barani humo