1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa wamalizika

14 Desemba 2007

NUSA DUA: Mkutano wa kimataifa juu ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani unamalizika leo hii Bali,nchini Indonesia.Wajumbe kutoka nchi 190 wanajitahadi kupata makubaliano juu ya njia za kuhifadhi mazingira.Marekani inashinikizwa na Umoja wa Ulaya kukubali rasmi kupunguza utoaji wa gesi zinazoathiri mazingira ifikapo mwaka 2020.

Waziri wa Mazingira wa Ujerumani,Sigmar Gabriel akihudhuria mkutano wa Bali amezishutumu Marekani na nchi zinazoinukia kiuchumi kuwa hazikounyesha ushujaa kufikia muafaka wa mazungumzo hayo.

Marekani lakini inasema,kila nchi iachiliwe kujiamulia kiwango cha kupunguzwa.Kwa upande mwingine,Naibu Rais wa zamani wa Marekani,Al Gore ameilaumu nchi yake kuwa inazuia maendeleo kupatikana katika majadiliano hayo.