Mkutano wa mabadiliko ya tabia-nchi wamalizika Bonn
17 Juni 2011Matangazo
Mkutano huu uliandaliwa na Umoja wa Matafa ulidhamiria kutafuta muafaka wa namna ambavyo mataifa yaliyoendelea na yanayoendelea yanavyoweza kushirikiana kuutimiza Mkataba wa Ulinzi wa Mazingira wa Kyoto, hasa katika suala zima la uzalishaji wa gesi-joto zinazohatarisha tabaka hewa na hivyo kuathiri mabadiliko ya tabia-nchi.
Mohammed Khelef amezungumza na mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Bwana Richard Muyungi, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira, anayeshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi, katika Ofisi ya Makamo wa Rais wa Tanzania, kuhusiana na mambo yaliyokubaliwa kwenye mkutano huo.
Mahojiano: Mohammed Khelef/Richard Muyungi
Mhariri: Othman Miraji