1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Biden na Xi, Je! Ujerumani iko mahala gani?

16 Novemba 2023

Dunia imefuatilia kwa karibu mkutano kati ya rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping.

USA Präsident Joe Biden und chinesischer Präsident Xi Jinping
Picha: Doug Mills/AP Photo/picture alliance

Uhusiano baina ya Marekani na China umo katika kiwango cha chini. Biashara ya usafirishaji bidhaa kati ya nchi hizo imepungua sana na ndio sababu dunia imefuatilia kwa karibu mkutano kati ya rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa China Xi Jinping.

Kushoto: Rais wa Marekani Joe Biden. Kulia Rais wa China Xi Jinping.Picha: Doug Mills/The New York Times/AP/picture alliance

Hata hivyo mwanazuoni Hanns Maull, kutoka majopo mawili ya watalaamu ya mjini Berlin anasema hakuna matumaini makubwa kutoka kwenye mkutano huo.

Amesema tunashuhudia sasa kuanzishwa tena mazungumzo lakini hiyo haina maana kwamba mazungumzo hayo yatawezesha kuondolewa sababu za mivutano kati ya China na Marekani. Bwana Maull ameongeza kusema kwamba pana maswala yanayohusu migogoro mizito na hakuna uhakika iwapo ufumbuzi utapatikana kwenye mazungumzo hayo.

Tathmini ya mtaalamu Josef Braml

Kwa mujibu wa tathmini ya mtaalamu kutoka Marekani Josef Braml, China na Marekani tayari zimo kwenye vita baridi na ameelezea wasiwasi wake kwamba mvutano wa kiuchumi unaweza kuvuruga ushirikiano unaohitajika kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na juhudi za kuepusha janga la uchafuzi wa mazingira.

Soma:Marais wa Marekani Joe Bden, na wa China Xi Jinping kukutana pembezoni mwa kutano wa APEC

Mvutano kati ya China na Marekani unaiweka Ujerumani katika hali ngumu kwa sababu katika upande mmoja Marekani ni mshirika muhimu wa Ujerumanikatika mambo ya usalama na kwa upande mwingine China ni mshirika mkuu wa kibiashara kwa Ujerumani.

Kutokana na kizungumkuti hicho, Ujerumani hivi karibuni ilifafanua sera yake juu ya China. Pamoja na mambo mengine sera hiyo inalenga shabaha ya Ujerumani kupunguza kuitegemea China. Wafanyabiashara wa Ujerumani wanatakiwa kutafuta masoko kwingineko.

Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Mwanazuoni Hanns Maull, kutoka majopo mawili ya watalaamu ya mjini Berlin amesema mvutano kati ya China na Marekani ni changamoto kubwa sio tu kwa Ujerumani bali pia kwa bara lote la Ulaya.

China na Marekani tayari zimo katika vita vya kiuchumi hata hivyo waziri wa biashara wa Marekani amesema nchi yake inataka biashara imara na China katika msingi wa haki.