Mkutano wa matayarisho wa kuunda serikali ya mseto Ujerumani
4 Januari 2018
Tuanze na gazeti la Rhine-Necker Zeitung la mjini Heidelberg , mhariri anazungumzia mkutano wa matayarisho ya kikao cha mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani kufuatia uchaguzi wa mwezi Septemba mwaka jana. Mhariri anaandika:
Ujerumani bado haina serikali rasmi hadi sasa na kama alivyosema kiongozi wa chama ndugu na chama tawala cha CDU , Horst Seehofer wa chama cha CSU kwamba hadi itakapofika wakati wa sikukuu ya pasaka serikali itakuwa imekwisha kamilika. Lakini hilo bado liko mbali sana. Hata kama kabla ya mkutano huu wa matayarisho, hali ya kuaminiana iliongezeka, maudhui juu ya mazungumzo hayo bado hayajapata muafaka. Kwa mfano suala la kubana sera za uhamiaji ambazo chama cha CSU kimewasilisha kama mapendekezo yake, hazipendelewi na chama cha SPD. Kumekuwa pia na hali ndogo ya kuwapo makubaliano kuhusu mageuzi katika bima ya afya. Merkel na Seehoffer wanapaswa kuridhia mengi zaidi iwapo wanataka serikali imara.
Gazeti la Reutlinger General-Anzeiger linazungumzia utafiti kuhusu sababu zinazopelekea wakimbizi kujihusisha na matukio ya uhalifu hapa nchini Ujerumani. Gazeti linaandika.
Hadi sasa haileti maana , kuwaweka wakimbizi wote katika kapu moja. Pamoja na hayo mtu hapaswi kufumbia macho matukio ya wakimbizi. Ujerumani inapaswa kufungua milango yake kwa wakimbizi wanaotoka katika mataifa yenye vita, lakini wale wakimbizi wanaokimbia nchi zao kutokana tu na umasikini ama wakimbizi wa kiuchumi hawapaswi kupewa matumaini ya kuishi hapa. kitu kinachosikitisha ni kwamba baadhi yao hujiingiza katika matendo ya kihalifu. Unaonesha utafiti. Kutokana na hilo ni sheria za uhamiaji zilizo wazi pekee ambazo zinaweza kuzuwia hali hiyo. Ukweli lakini ni kwamba, taifa na jamii wanapaswa kufanya zaidi kwa wakimbizi ambao hawana nafasi ya kubakia warejeshwe makwao. Hii sio chuki dhidi ya watu kutoka nje, lakini ni ishara ya kujilinda kidemokrasia.
Nalo gazeti la Hannoversche Allgemeine , likizungumzia mada hiyo linaandika:
Itabidi kutafuta haraka kampuni itakayowashughulikia wakimbizi. ambayo inaweka wazi kwamba , yeyote atakayefuata sheria anaweza hata akaileta familia yake. Kwa yule ambaye atafuata sheria , na hii itaanzia kwa yule ambaye hajatoa utambulisho wa uongo, atapewa fedha mara mbili zaidi, na hatojihusisha na udhalilishaji wa wanawake ama matukio ya kihalifu. Wale wataoapatikana na hatia kama hizo haraka watarejeshwa makwao. Hii itawafanya wakimbizi vijana kufuata sheria na kuwatuliza. Yule atakayefuata sheria atapewa fursa .
Kuhusu maandamano yaliyotokea nchini Iran gazeti la Märkische Oderzeitung la mjini Frankfurt linaandika.
Tofauti na mwaka 2009 vijana wa tabaka la kati hawakupambana mara hii katika miji mikubwa kuhusu udanganyifu katika uchaguzi, na waandamanaji hawakuwa na uongozi wa kisiasa. Pamoja na hayo mapambano dhidi ya watawala yanaendelea kubaki bila mwelekeo , na hali inaendelea kuwa vile vile ambapo watawala bado hawajaweza kuwasikiliza raia wao. Mbali ya hivyo , bajeti ya taifa inapaswa kugawanywa kwa usawa, ili iwafikie wote na kupunguza mzigo wa wakimbizi kutoka Iran kwenda katika mataifa jirani ya Kiarabu.
Mwandishi: Sekione Kitojo / inlandspresse
Mhariri: Gakuba, Daniel