1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Mazingira mjini Durban wamalizika kwa mafanikio

12 Desemba 2011

Mkutano mrefu kabisa wa mabadiliko ya tabia nchi kuwahi kushuhudiwa umemalizika jana mjini Durban kwa kupatikana makubaliano juu ya mkataba mpya kuhusu utoaji gesi chafu zinazoharibu mazingira.

epa03028144 YEARENDER 2011 NOVEMBER Cyclists power lights on an installation depicting a Baobab tree part of a renewable energies display on Durban's beachfront during the COP 17 / CMP 7 United Nations (UN) Climate Change Conference 2011 in Durban, South Africa, 29 November 2011. COP 17 is the 17th session of the Congress of the Parties (COP) comprising 194 countries meeting to discuss the United Nations Framework Convention on Climate Change (UNFCCC) between 28 November and 09 December 2011. EPA/NIC BOTHMA +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mafanikio yapatikana katika mkutano wa DurbanPicha: picture-alliance/dpa

 Wajumbe kutoka mataifa 194 hatimae walifikia makubaliano  na kuondoa hofu iliokuweko kwamba huenda mkutano huo wa Umoja wa mataifa ungeshindwa.  Mkataba huo sasa umeuokoa ule mkataba wa  Kyoto.

Wiki mbili za  majadiliano marefu hatimae zilizaa matunda jana na hivyo mkutano huo wa Umoja wa mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kumalizika mjini Durban Afrika kusini kwa mafanikio kwa tangazo  la mkuu wa Umoja wa mataifa anayehusika na suala hilo Bibi Christiana Figueres.Makubaliano yalifikiwa dakika ya mwisho kutokana na  muda wa masaa 30 ya nyongeza, uliofuatia wito wa mwenyekiti wake , Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Afrika kusini Naite Nkoana Mashabane ambaye  akizungumzia  juu ya haja ya kupatikana makubaliano

 alisema :

"Nafikiri tumetambua kwamba si barabara. na tusiruhusu kisichokuwa barabara  kuharibu kizuri na kinachowezekana ."

Christiana Figueres mwakilishi wa umoja wa mataifa kuhusu mazingira.Picha: AP

Waziri Mashabane alikuwa akitoa wito kwa wajumbe kuzingatia umuhimu wa kuafikiana.

Hivi sasa kile kinachojulikana kama  jukwaa la Durban, limefungua njia ya kuanza utaratibu wa kuwa  na sera ya  dunia juu ya mabadiliko ya tabia nchi, itakayoongoza juhudi za kupunguza utoaji gesi zinazochafua mazingira katika kipindi cha miaka 10 ijayo, ili kiwango cha joto kibakie katika kipimo cha gredi mbili Celsius. Wachambuzi wanasema kutokana na sera ya sasa kiwango hicho cha joto  ni  katika kipimo cha gredi nne celsius.

Mkataba mpya kwa hivyo unaweka mpango wa mabadiliko ya tabia nchi hadi 2017 au 2020, ambapo sio tu nchi zilizoendelea kiviwanda zitakazotakiwa kuwajibika  bali hata nchi zinazoendelea nazo zitakuwa na wajibu wa kupunguza utoaji wa  gesi zinazochafua mazingira.

Umoja wa Ulaya kwa upande wake uliungana na  wanaharakati duniani kukaribisha mafanikio hayo, lakini ukasema dunia itahitaji mpango mkubwa zaidi kupunguza utoaji wa gesi zinazochafua mazingira, kuliko ilivyokuwa  katika  mkataba wa  awali wa Kyoto.

Licha ya kwamba makubaliano ya Durban si muafaka kabisa lakini ni hatua moja kubwa mbele. Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na mazingira Connie Hedegaard  amesema :

"Unapokuwa na  tatizo kubwa, Unatpokuwa na tatizo la dunia,  tatizo la kimataifa. basi hatua sa hiyari huwa hazitoshi kulitatuwa tatizo hilo."

Bibi Connie Hedegaard katika mkutano wa MazingiraPicha: picture-alliance/dpa

Mkutano wa Durban ulifikia tamati na kutoa matumaini  kutokana na maridhiano  hasa kati ya India na Umoja wa Ulaya chini ya usimamizi wa mwenyekiti wa mkutano huo Bibi Mashabane.

Durban imezaa ushirikiana mpya kati ya nchi zinazoendelea  na Umoja wa Ulaya katika kukabiliana na ongezeko la ujoto duniani.

Mtaalamu wa Shirika la mazingira la Greenpeace Martin Kaiser amesema,Ni jambo  zuri kuona China, India  ,Brazil na Afrika kusini zikishirikiana  ana hatimae kufanikisha kupatikana kwa mkataba mpya kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Miaka mitano ijayo itatoa sura ya awali ya  kule dunia inakoelekea.

Mwandishi: Jeppessen Halle/  ZR/ Moahammed Abdul-Rahman

Mhariri: Othman Miraji

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW