1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mkutano wa NATO kuanza Jumanne nchini Lithuania

10 Julai 2023

Viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanaelekea nchini Lithuania kwa mkutano wa kilele wa siku mbili unaoanza kesho ambao utatawaliwa na ajenda ya vita nchini Ukraine.

Lithuania, Vilnius | NATO
Maandalizi ya mkutano wa kilele wa NATOPicha: Sean Gallup/Getty Images

Viongozi wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO wanaelekea nchini Lithuania kwa mkutano wa kilele wa siku mbili unaoanza kesho ambao utatawaliwa na ajenda ya vita nchini Ukraine pamoja na hatma ya uanachama wa Sweden ndani ya muungano huo. Shinikizo la Ukraine la kutaka ikaribishwe haraka ndani ya NATO pia litajadiliwa lakini duru kadhaa zimearifu kwamba nchi 31wanachama wa NATO huenda watarefusha mpango huo.

Ama kuhusu suala la uanachama wa Sweden, viongozi wa jumuiya hiyo watautumia mkutano wa mjini Vilnius kujaribu kumaliza tofauti kati ya nchi hiyo na Uturuki inayokataa hadi sasa kuidhinisha ombi lake.

Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema kuna matumaini mwafaka unaweza kupatikana katika wakati viongozi wa nchi hizo mbili watakuwa na mkutano hii leo kushughulikia wasiwasi wa Uturuki uliosababisha kuzuia uanachama wa Sweden. Serikali mjini Ankara inaituhumu Sweden kufadhili shughuli za makundi yanatoshia usalama wa Uturuki hususani yale ya jamii ya Wakurdi.