Mkutano wa OSCE .
2 Desemba 2010Viongozi wa dunia wametoa wito wa pamoja wa kuwepo shirika lenye nguvu la usalama na ushirikiano Ulaya, OSCE, katika mkutano wa kwanza wa shirika hilo tangu mwaka 1999 nchini Kazakhstan.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema shirika hilo lenye wanachama 56 lazima kwanza lihakikishe amani na uhuru inakuwepo katika mipaka yake. Akiigusia nchi mwenyeji, Merkel amesema hakikisho la haki za binaadamu na uhuru wa kujieleza na wa vyombo vya habari, ni lazima utekelezwe.
Kazakhstan ni nchi ya kwanza ya iliyokuwa muungano wa Sovieti kushikilia uwenyekiti wa shirika hilo. Waandishi wa habari wasio na mipaka wamesema nchi hiyo haifai kuandaa mkutano huo kwani haifikii viwango vya shirika hilo.
OSCE liliundwa wakati wa vita baridi kama njia ya majadiliano kati ya mataifa ya kikomyunisti na Magharibi.
Mwandishi Maryam Abdalla/DPAE