Viongozi wa nchi 14 wanachama wa Jumuiya ya ushirikiano wa maendeleo kusini mwa Afrika (SADC), wanatarajiwa kukutana mjini Dar es Salaam,Tanzania, katika kikao cha dharura kitakachojadili hali ya siasa na usalama katika eneo hilo pamoja na matukio nchini Zimbabwe.
Matangazo
Taarifa inasema Robert Mugabe wa Zimbabwe anatarajiwa kuhudhuria mkutano huo.
Kutoka Dar es Salaam, mwandishi wetu Badra Masoud ametuletea ripoti zaidi juu ya mkutano huo.