Mkutano wa siri wa Nentanyahuna John Kelly
20 Februari 2017Mkutano huo uliohudhuriwa pia na mfalme Abdallah II wa Jordan na rais wa Misri Abdel Fattah el Sissi, ulipendekeza kutafuta amani baina ya Israel na Palestina. Lakini Netanyahu, alilikataa pendekezo hilo ambalo liliungwa mkono na nchi za kiarabu. Kutokana na maafisa wa utawala wa rais wa zamani Barack Obama, Kerry alipendekeza nchi za mashariki ya kati kuitambua Israel kama dola la kiyahudi. Lakini Netanyahu alikata pendekezo hilo, ambalo lingelazimisha Israel kuondoka katika sehemu ambazo tayari zinamilikiwa na Israel .
Katika mageuzi yaliopendekezwa katika mkutano huo, nipamoja na yale ya nchi za kiarabu kutambua kuwa Israel ni dola la kiyahudi, kutambua pia kuwa Jerusalem ni mji mkuu wa pande zote mbili yaani Israel na Palestina na haki ya kurejea kwa wakimbizi wa kipalestina katika maeneo waliyoyapoteza ndani ya kile kinachojulikana hii leo kama taifa la Israel. Mjumbe mmoja alisema kuwa sababu kubwa ya mkutano huo ilikuwa kuanzisha tena mazungumzo ya amani ya mashariki ya kati ambayo Netanyahu mwenyewe alitaka yawepo .
Juhudi zilizopendekezwa katika mkutanohuo wa siri
Juhudi hizo pia zilionekana kuwa msingi wa mazungumzo yaliodumu muda mfupi na Kiongozi wa upinzani mwenye msimamo wa wastani Isaac Herzog alipokuwa ajiunge na serikali ya Netanyahu. Lakini mpango huo ukavunjika haraka, wakati Netanyahu alipomjumuisha katika serikali yake kiongozi mwenye msimamo wa Kizalendo wa siasa kali za mrengo wa kulia Avigdor Lieberman na kumpa uwaziri wa ulinzi.
Netanyahu hakuzungumzia kabisa ripoti hiyo ya mkutano huo wa siri katika mkutano wake wa kila wiki na baraza lake la mawaziri, na ofisi yake pia imekataaa kusema chochote juu ya mkutano huo .
Katika mkutano wake wa kwanza na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Washington , Netanyahu alisema kuwa
" Kuna siku mpya na ni siku nzuri ." Akimaaanisha mapokezi mazuri aliyoyapata alipofika Ikula ya White House. Lakini mara hali hio ilibadilika pale tuTrump alipomuomba Netanyahu kusimamisha kwa muda kidogo ujenzi wa makaazi ya kiyahudi katika sehemu zinazokaliwa na Israel katika maeneo ya wapalestina. Waziri wa ulinzi wa Israel Lieberman, alisema kuwa kwake yeye kuundwa dola ya Palestine ndio suluhisho muafaka.
"Mtazamo wangu ni kumaliza mgogoro huu na suluhuu ni kuwepo kwa dola mbili-Israel na Palestina . Naamini ni muhimu kwetu kuwepo kwa dola yaa kiyahudi ," . Libermann aliyasema hayo wakati akihutubia mkutano wa usalama mjini Munich mwishoni mwa juma lililopita.
Mwandishi : Najma Said/APE /EAP
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman