Mkutano wa Usalama wa Munich 2026 wahitimishwa Jumapili
16 Februari 2026
Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amesema Marekani haina nia ya kuifanya Ulaya kuwa "kibaraka" , lakini mshirika ambaye atakuwa tayari kuunga mkono maono ya Rais Donald Trump ya "kufufua" utaratibu wa kimataifa.
Hata hivyo, mkutano huo wa Munich ulishuhudia ukosoaji hasa kuhusu nafasi na ushiriki mdogo wa bara la Afrika, hasa kutokana na kuwa mijadala katika mkutano huo haikuangazia kwa kina migogoro inayoikumba Afrika kama vile Sudan, mashariki mwa DRC, au katika kanda ya Sahel.