1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa viongozi wa mataifa ya waislamu waanza Malaysia.

Admin.WagnerD18 Desemba 2019

Viongozi na wawakilishi wa ngazi ya juu kutoka karibu mataifa 20 yenye idadi kubwa ya waislamu duniani wanakusanyika leo mjini Kuala Lumpur, Malaysia, kujadili masuala yanayowatia misukosuko waislamu kote ulimwenguni.

Malaysia Erdogan zu Besuch
Rais Reccep Tayyip Erdogan akiwasili Kuala Lumpur kwa mkutano wa viongozi wa mataifa ya kiislamu.Picha: picture-alliance/AA/Presidency of Turkey/M. Cetinmuhurdar

Duru kutoka nchini Malaysia zinasema hakuna ajenda zilizotolewa kwa ajili ya mkutano wa mjini Kuala Lumpur lakini viongozi wanaokutana wanaweza kuzungumzia masuala chungu nzima yanayokabili jamii za waislamu kote ulimwenguni.

Mkutano huo unaweza kuzungumzia mivutano ya muda mrefu ikiwemo suala la jimbo la Kashmir na mizozo katika eneo la mashariki ya kati ikiwemo ule wa Syria na Yemen.

Kadhalika hali dhaifu na ukatili unaoikabili jamii ndogo ya waislamu wa Rohingya nchini Myanmar na hasira inayoongezeka kuhusiana na kambi za China zinazowahifadhi waumini wa jamii ya wachache ya waislamu wa Uighur yanaweza pia kuwa masuala muhimu wakati wa mkutano wa Kuala Lumpur.

Viongozi hao wanaweza vile vile kujadili njia za kuzuia ongezeko la mitazamo hasi dhidi ya Uislamu duniani.

Waziri mkuu wa Malaysia Mahathir Mohamad na rais wa Uturuki Tayyip Erdogan, miongoni mwa viongozi walio na ujasiri wa kuzungumzia kwa uwazi masuala mbalimbali duniani, wamepangiwa kutoa hotuba wakati wa mkutano huo wa siku nne unaotarajiwa kufikia kelele Jumamosi inayokuja.

Pakistan haitohudhuria mkutano huo 

Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan hatohudhuria mkutano wa Kuala LumpurPicha: Reuters/J. lee

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan, ambaye pamoja na Mahathir na Erdogan walishajihisha kuitishwa mkutano wa Kuala Lumpur, alifikia uamuzi wa saa za mwisho wa kutohudhuria mkutano huo.

Baadhi ya maafisa wa Pakistan ambao hawakutaka majina yao kutajwa, wamesema uamuzi wa Khan umetokana na shinikizo la Saudi Arabia lakini vyombo vya habari vya nchi hiyo vimewanukuu wasaidizi wake wakisema hoja hiyo haina ukweli.

Rais wa Iran Hassan Rouhani na Amirivwa Qatar Sheikh Tamim bin Hamid Al-Thani, viongozi wa mataifa yaliyo na mahusiano duni na Saudi Arabia ni miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo.

Saudi Arabia yasusia mkutano wa Kuala Lumpur

Mfalme Salman wa Saudi ArabiaPicha: AFP/Saudi Royal Palace/B. al-Jaloud

Saudia Arabia ambayo imetangaza kuususia imesema mkutano wa Kuala Lumpur siyo jukwaa sahihi la kuzungumzia masuala muhimu yanayowahusu wailsam bilioni 1.7 duniani.

Hata hivyo wachambuzi wa masuala ya siasa wameshuku kuwa Saudi Arabia imehofia kutengwa kidiplomasia wakati wa mkutano huo na mahasimu zake wa jadi ambayo ni mataifa ya Qatar, Iran  na Uturuki

Shirika la habari la Saudi Arabia limeripoti kwamba wakati wa mazungumzo ya simu yaliyofanyika jana Mfalme Salman wa Saudia alimwambia waziri mkuu wa Malaysia kuwa masuala yanayohusu waislamu yanapaswa kujadiliwa kupitia Jumuiya ya Ushirikiano wa mataifa ya kiislamu, OIC.

Kukosekana kwa Saudi Arabia, kitovu cha dini ya kiislamu na mabyo mfalme wake ndiye mhifadhi mkuu wa misikiti miwili mitakatifu ya Makka na Madina kunadhiririsha kuwepo miganyiko katika ulimwengu wa kiislamu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW