Mkutano wa Wakfu wa Jimmy Carter mjini Addis Abeba,Ethiopia
14 Februari 2007
Mjini Addis Abeba,Ethiopia, wiki hii kunafanyika mkutano kuhusu mafundisho katika sekta ya afya. Mkutano huu uliandaliwa na wakfu wa Jimmy Carter, rais wa zamani wa Marekani, ambaye mwenyewe amewasili Addis Abeba kuhutubia mkutano huo. Mwandishi wetu wa Addis Abeba, Anaclet Rwegayura alisikiliza hotuba hiyo.