Mkutano wa Wakuu wa Majeshi wa maziwa makuu mjini Bujumbura
23 Aprili 2008
Wakuu wa majeshi kutoka nchi nne za maziwa makuu, Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, Rwanda, Uganda na Burundi wamemaliza mkutano wao wa siku moja mjini Bujumbura.
Matangazo
Lengo ni kuendeleza juhudi za kuyatokomeza makundi ya waasi yanayovuruga usalama wa eneo hilo zima la maziwa makuu.
Kutoka mji mkuu huo wa Burundi mwandishi wetu Gregoire Nijimbere ana ripoti kamili.