1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkutano wa Wiki ya Maji waanza Sweden

Mohamed Dahman18 Agosti 2008

Takriban wataalamu 2,500 wanakutana mjini Stockholm Sweden wiki hii kuweka katika nadhari mojawapo ya masuala yanayohitaji utatuzi wa haraka ambayo ni rasilmali za maji.

Muumini wa Kibaniani akinywa maji wakati mwanamke akifua nguo licha ya kuwepo kwa maua na taka ziliizoachwa na wafanya ziara ya kidini huko Sangam ambapo mto Ganges unakutana na Yamuna, huko Allahabad nchini India.Picha: AP

Mada ya mkutano huo wa kila mwaka,mwaka huu ni masuala ya udhibiti afya wa kuondowa maji taka na takataka na kuweka usafi.

Takriban watu bilioni mbili na milioni sita duniani hawana vyoo safi hiyo ni kama asilimia 40 ya idadi ya watu duniani.Watu wengine bilioni moja wanaishi bila ya kuwa na maji safi ya kunywa. Matokeo yake ni maafa, kila sekunde 20 mtoto huafariki kutokana na kipindu pindi au na magonjwa yanayosababishwa na maji machafu.

Takriban watu wengi wanaokosa mahitaji ya msingi ya udhibiti afya,uondowaji maji taka, takataka na ukosefu wa vyoo safi wanaishi Barani Asia. Nchini India pekee watu milioni 750 hufanya haja hadharani katika maeneo ya wazi kutokana na ukosefu wa vyoo.

Maziwa na maji yalioko ardhini yamechafuliwa na vijidudu na taka taka.Mfumo wa maji taka haufanyi kazi kabisa au mitambo ya kusafisha maji na kwa ajili hiyo watu wengi hupoteza maisha yao anasema mkuu wa Kituo cha Maji na Mazingira nchini India Sunita Narain.

(O-Ton Narain)

Tuko wazi kwamba iwapo hatutoyashughulikia maji, iwapo hatutowapatia watu maji safi hapo tena huo unakuwa mzigo mkubwa kwa afya.Na hata hivi sasa maradhi yanayotokana na maji machafu bado ni sababu kuu ya vifo kwa kadri watoto wanavyohusika.

Katika nchi zinazoendelea na zile zinazoinukia kiuchumi mara nyingi watoto walio na umri wa chini ya miaka sita hufariki kutokana na kunywa maji yaliochafuliwa.

Takriban nusu ya idadi ya watu duniani wana ukosefu wa vyoo safi hali ambayo inaweza kuwa na matokeo mabaya sana kama iivyothibitishwa kwa afya ya binaadamu na ambayo inatowa changamoto katika kulitatuwa tatizo hilo kutokana na maji kuzidi kuwa rasilmali adimu.

Mabadiliko ya hali ya hewa ,kuongezeka kwa idadi ya watu duniani na maendeleo ya kiuchumi ya haraka barani Asia na Afrika yote hayo yameweka mzigo mkubwa kwa maji.

John Lange ni kiongozi wa Baraza la Kimataifa la Usambazaji Maji na Ushikiano wa Udhibiti Afya wa kuondowa maji taka na takataka.

(O-TON Lange)

Dhana ni kwamba watu waboreshe udibiti afya wao wa kuondowa maji taka na takataka na kuweka usafi wa vyoo kutakakoshuhudia ujengaji wa vyoo vya lindi au vyoo vya aina fulani ni muhimu sio tu kwa ajili ya nyumba zao wenyewe na zile za familia bali kwa faida ya jamii nzima.Iwapo watu wanatambuwa uchafu wa mitaro ya majirani zao unaatihri nyumba zao huleta motisha kwa jamii kukusanyika pamoja kuboresha usafi wa mazingira hayo na kuboresha maisha yao kwa jumla.

Asilimia 30 ya idadi ya watu duniani katika nchi 30 wanakabiliwa na uhaba wa maji idadi ambayo inategemewa kufikia asilimia 30 ifikapo mwaka 2025 kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao umeutangaza mwaka 2008 kuwa Mwaka wa Kimataifa wa Udhibiti Afya wa kuondowa maji taka na takataka na kuweka vyoo safi na usafi wa mazingira kwa jumla.

Mkutano wa Wiki ya Maji ambao umeanza leo hii umepewa jina Maendeleo na Matarajio kwa Maji Kwa ajili ya Dunia ilio Safi na yenye Afya hususan utalenga juu ya hatari za ukosefu wa vyoo vya kutosha na usafi kwa watu bilioni mbili milioni sita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW