1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCameroon

Mkutano wa WTO wamalizika bila maafikiano

30 Machi 2026

Mkutano wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) umemalizika nchini Kameruni bila ya makubaliano kwenye masuala muhimu ya mageuzi, kilimo na biashara ya mtandaoni kutokana na mgongano baina ya Marekani na Brazil.

Ngozi Okonjo-Iweala | WTO
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO), Ngozi Okonjo-Iweala, anasema Marekani na Brazil zinatakiwa kumaliza tafauti zao.Picha: DW

Waziri wa Biashara wa Kameruni, Mbarga Atangana, alisema baada ya siku nne za mkutano huo mjini Yaoundé, wameona muda hautoshi kufikia makubaliano kwenye masuala hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa WTO,  Ngozi Okonjo-Iweala, alisema anatumai nchi hizo "zitaweza kuurejesha mkataba wa kusitishwa kwa biashara ya mtandaoni ambao umemalizika muda wake, na kuziwezesha kutoza ushuru wa forodha kwenye utumaji wa kielektroniki kama vile kupakua na kutangaza."

Majadiliano hayo yalikwama baada ya Marekani na Brazil kutafautiana juu ya kuongezwa muda huo kwa miaka miwili mingine.

Hata hivyo, mkurugenzi mkuu huyo wa WTO aliongeza kuwa Marekani na Brazil zilikuwa zinafanya mazungumzo baina yao kuukwamua mkwamo huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW