1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Mkuu mpya wa majeshi Pakistan aanza rasmi majukumu yake

29 Novemba 2022

Jenerali Asim Munir aliyeteuliwa mkuu mpya wa majeshi Pakistan ameanza majukumu yake katika kipindi ambacho kinashuhudia ongezeko la mpasuko wa kisiasa kati ya serikali na kiongozi wa upinzani mwenye umaarufu Imran Khan.

Pakistan | General Syed Asim Muni
Picha: W.K. Yousufzai/AP/picture alliance

Khan aliyekuwa mchezaji wa Kriketi na kisha kuingia kwenye siasa na ambaye aliondolewa kwa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani nae bungeni,  amemtaka mkuu huyo mpya wa majeshi kuumaliza mkwamo wa kisiasa unaoendelea nchini humo. 

Aidha mkuu wa Majeshi Asim Munir anaanza majukumu yake kukiweko pia kitisho kipya kutoka kundi kubwa la wanamgambo ambalo limehusika kwa miaka 15 na msururu wa mashambulio ya umwagaji damu.

Katika historia ya Pakistan jeshi lina usemi kwa kiasi kikubwa likiwa limeendesha utawala kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 katika historia ya miaka 75 ya nchi hiyo.Munir, aliyekuwa mkuu wa shughuli za ujasusi anachukua mahala pa jenerali Javed Bajwa aliyemaliza muda wake wa miaka sita.