Mkuu wa al-Qaeda Afrika Mashariki ameuawa
12 Juni 2011Matangazo
Waziri Clinton, alipozungumza na waandishi wa habari akiwa ziarani nchini Tanzania, alisema kifo cha Fazul Abdullah ni " pigo kubwa" kwa al-Qaeda na washirika wake katika eneo la Afrika Mashariki.
Fazul aliekuwa akitazamwa kama kiongozi wa al-Qaeda katika eneo la Afrika Mashariki, aliuawa jumanne iliyopita mjini Mogadishu. Fazul aliekuwa na umri wa miaka 38, alikuwa akisakwa kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi katika balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania mwaka 1998, yaliyosababisha vifo vya watu 224.
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Prema Martin