1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa Bunge la EU aonya kuongezeka msimamo mkali Ujerumani

23 Novemba 2024

Rais wa Bunge la Ulaya, Roberta Metsola ameonesha wasiwasi juu ya uwezekano wa vyama vya siasa kali kupata nguvu kubwa ya kisiasa katika bunge lijalo la Ujerumani.

Rais wa Bunge la Brussels EU Metsola na Zelenskyj
Rais wa Bunge la Ulaya Roberta Metsola akizungumza mjini Brussels Novemba 19, 2024.Picha: NICOLAS TUCAT/AFP

Na amehoji hali hiyo itakuwa na tafsri gani kwa Ulaya. Kutokana na mashaka yake hayo ametoa wito kwa vyama vya Ujerumani vinavyounga mkono  Umoja wa Ulaya kusimama pamoja katika masuala muhimu. Ameelezea wasiwasi wake baada ya uchaguzi wa majimbo katika eneo lililokuwa Ujerumani Mashariki. Metsola amesema kuongezeka kwa wafuasi wa siasa kali katika eneo hilo la iliyokuwa Ujerumani Mashariki kwenye uchaguzi wa majimbo matatu mwezi Septemba ulitoa onyo kwa matokeo yaliokipa nguvu chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, AfD. Chama cha BSW pia kilifaulu kuongeza wafuasi katika maeneo hayo ambapo kilitwaa nafasi ya tatu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW