Mkuu wa chama cha soka Rwanda akamatwa
11 Juni 2010Matangazo
Jeshi la Rwanda limetangaza kuwa limemkamata na kumtia jela Rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini humo, FERWAFA, Brigadia Jenerali John Bosco Kazura. Msemaji wa jeshi hilo ametangaza mjini Kigali kuwa rais huyo wa FERWAFA alifanya makosa ya kwenda nje ya nchi bila kibali cha wakubwa wake. Jenerali Kazura inasemekana alikuwa amekwenda Afrika ya Kusini kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa kombe la dunia ambalo limeanza leo. Yeye ni afisa wa tatu wa cheo cha jenerali kutiwa kizimbani kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Daniel Gakuba anayo maelezo zaidi kutoka Kigali.