1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaEthiopia

Mkuu wa chama tawala Amhara auwawa

28 Aprili 2023

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ametangaza kuwa mkuu wa chama chake tawala cha Prosperity Party katika eneo la kaskazini la Amhara ameuwawa.

Äthiopien Wiederaufnahme der Transportdienste in Bahirdar
Picha: Alemnew Mekonnen/DW

Kulingana na serikali ya Amhara, Girma Yeshitila, alikuwa miongoni mwa watu watano waliouwawa katika shambulizi lililofanywa mchana wa jana walipokuwa njiani kuelekea katika mojawapo ya miji ya jimbo hilo.

Katika ujumbe aliouandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook, Waziri Mkuu Abiy amewalaumu watu wenye itikadi kali kwa mauaji hayo akisemaYeshitila ameuwawa na watu ambao hawakuweza kushinda  kwa kueleza mawazo yao.

Mkuu huyo wa chama alikuwa akilengwa mara kwa mara na wazalendo wa Amhara katika mitandao ya kijamii, wakimtaja kuwa ni msaliti kutokana na ukaribu aliokuwa nao na Abiy Ahmed.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW