SiasaAsia
Mkuu wa chama tawala Korea Kusini 'amgeuka' rais
6 Desemba 2024Matangazo
Han Dong-hoon anayeongoza chama cha People Power, amesema ikiwa Rais Yoon ataendelea kubakia madarakani, huenda hatua kali kama vile sheria ya matumizi ya nguvu za kijeshi, zinaweza kurejea, na hivyo kuiweka Jamhuri ya Korea na raia wake hatarini.
Mkuu huyo wa chama tawala amesema pia kwamba lazima madaraka ya kikatiba ya Rais Yoon yasimamishwe.
Soma zaidi: Chama tawala Korea Kusini chaahidi kupinga kumuondoa rais
Han amesema Rais Yoon alikuwa ameagiza kukamatwa kwa wanasiasa wakubwa kwa madai kwamba wanapinga serikali.
Kauli hii huenda inamaanisha kuwa chama hicho tawala kitabadilisha msimamo wake wa awali wa kuwaagiza wabunge wake kuzuwia kura ya kutokuwa na imani iliyopendekezwa na upinzani.