1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mkuu wa IAEA akitembelea kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia

Daniel Gakuba
29 Machi 2023

Mkuu wa shirika la kimataifa la kudhibiti nishati ya atomiki IAEA, Rafael Grossi anakitembelea leo kinu cha nyuklia cha Ukraine cha Zaporizhzhia.

Ukraine Saporischschja | Präsident Wolodymyr Selenskyj & UN-Atomenergiechef Rafael Grossi
Picha: Efrem Lukatsky/AP Photo/picture alliance

Rafael Grossi ambaye hii ni mara yake ya pili kukizuru kinu hicho tangu kilipokamatwa na wanajeshi wa Urusi mwaka uliopita, anasema ziara hii inakwenda sambamba na juhudi za kupunguza uwezekano wa kutokea ajali.

Urusi na Ukraine zimekuwa zikishutumiana kukishambulia kwa mizinga kinu cha Zaporizhzhia, na mkuu huyu wa shirika la IAEA amekuwa akizitaka nchi hizo mbili kufikia makubaliano ya kukilinda kituo hicho cha kinyuklia ambacho ndicho kikubwa zaidi barani Ulaya. Wakaguzi wa IAEA wamewekwa katika kinu hicho tangu mwaka jana, kufuatia hofu juu ya uwezekano wa kutokea mkasa mkubwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW