Mkuu wa jeshi la Israel Meja Jenerali Herzi Halevi ajiuzulu
21 Januari 2025Matangazo
Katika barua ya kujiuzulu kwake ametowa ufafanuzi juu ya sababu za kujiuzulu kwake akikiri kushindwa kwake kuzuia uvamizi wa Oktoba 7 na kusema kwamba anaondoka katika wakati ambapo yamepatikana mafanikio katika jeshi hilo la Israel.
Aidha kiongozi wa upinzani wa Israek Yair Lapid ameitaka serikali ya waziri mkuu Benjamin Netanyahu ijiuzulu baada ya Halevi kujiuzulu.
Baraza la mawaziri la Israel laidhinisha makubaliano ya kusitisha mapigano.
Wakati huohuo Israel imeanzisha operesheni kubwa ya kijeshi katika mji unaokaliwa kwa mabavu na nchi hiyo wa Jenin,katika Ukingo wa Magharibi.Wizara ya afya ya Palestina imesema takriban watu sita wameuwawa na 35 wamejeruhiwa.