1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Al-Burhan asema hatoshiriki mazungumzo ya amani Uswisi

26 Agosti 2024

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan amesema kuwa serikali yake haitajiunga na mazungumzo ya amani na kikosi cha wanamgambo RSF yanayofanyika nchini Uswisi.

Sudan | Vorsitzender des Souveränen Rates des Sudan | Abdel Fattah al-Burhan
Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-BurhanPicha: AFP

Al-Burhan badala yake ameapa kuendelea kupigana hata kwa muda wa miaka 100.

Mkuu huyo wa jeshi la Sudan ambaye vikosi vyake vimekuwa vikipambana na wanamgambo wa RSF kwa zaidi ya miezi 16, amewaambia waandishi wa habari mjini Port Sudan kuwa hawatokwenda Geneva kwa ajili ya kushiriki mazungumzo ya amani.

Soma pia: Sudan yakumbwa na mlipuko wa kipindupindu

Marekani ilianzisha mazungumzo nchini Uswisi mnamo Agosti 14 yaliyolenga kupunguza mateso wanayopitia raia wa Sudan na kufanikisha kusitishwa kwa mapigano.

Licha ya RSF kushiriki kwenye mazungumzo hayo, jeshi la Sudan linaripotiwa kutoridishwa na muundo wa mazungumzo hayo na likaamua kususia, ingawa limekuwa likifanya mazungumzo kwa njia ya simu na wapatanishi.