SiasaUganda
Mkuu wa jeshi la Uganda amtishia kifo kiongozi wa upinzani
21 Januari 2026
Matangazo
Jenerali Muhoozi Kainerugaba aliandika kwenye mtandao wa X siku ya Jumanne (Januari 20) kwamba walikuwa wamewauwa wale aliowaita magaidi 22 wa chama cha NUP (cha Bobi Wine) na kwamba anatazamia "wa 23 atakuwa Kabobi!"
Kiongozi huyo wa upinzani, ambaye aliwania urais kupingana na Museveni, alitangazwa na tume ya uchaguzi kushindwa na Museveni, na tangu Jumamosi amekuwa mafichoni baada ya kuvishutumu vikosi vya usalama kutaka kumteka.
Kainerugaba alimpa Wine masaa 48 ya kujisalimisha ama akabiliwe na hatua kama muasi.
Mwenyewe Wine aliandika kwenye mitandao ya kijamii kulitaka jeshi kuondoka kwenye nyumba yake, ambako alisema familia yake haikuwa salama.