Mkuu wa misaada wa UN asifu mkutano wake na Burhan
12 Novemba 2025
Mkutano huo ulikuwa ni wa kuhakikisha kuwa misaadamuhimu inafika katika kila kona ya nchi hiyo iliyozongwa na mapigano.
Fletcher alikutana na Burhan katika mji wa Port Sudan.
"Mzozo wa kiutu nchini Sudan uko katika viwango vya kushtusha na kama nilivyosema katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita, jamii ya kimataifa imeshtushwa na ukatili unaofanywa El-Fasher. Sote tunataka kuona amani ikirejea kwa Wasudan na jamii ya kiutu iko tayari kuongeza na kufikisha misaada ya kuokoa maisha kwa mamilioni ya watu wa Sudan wapate chakula na madawa," alisema Fletcher.
Jeshi la Sudan linasema wakati wa mkutano huo, Burhan alisisitiza haja ya mashirika ya Umoja wa Mataifa kuheshimu uhuru wa Sudan na maslahi ya kitaifa ya nchi hiyo, ukizingatia yaliyotokea katika mji wa El-Fasher.
Wizara ya mambo ya nje ya Misri inasema Fletcher alikutana pia na maafisa wa nchi hiyo kujadili njia za kuongeza usmabazaji wa misaada.