1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NATO yaikosoa China kwa kususia mkutano wa amani kwa Ukraine

5 Juni 2024

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg, ameikosoa China kwa kuamua kususia mkutano wa amani kwa Ukraine utakaofanyika nchini Uswisi baadaye mwezi huu.

Prag | NATO Generalsekretär Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg akihutubia mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano usio rasmi wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO huko Prague, Jamhuri ya Czech Mei 31, 2024.Picha: Peter David Josek/AFP/Getty Images

Katika mahojiano na shirika la utangazaji la Ujerumani, NDR, Stoltenberg, alisema inasikitisha kwamba China iliamua kutoshiriki mkutano huo. Uswisi imezialika takribani nchi 160 kwenye mkutano huo utakaofanyika tarehe 15 na 16 mwezi huu kujadili njia za kupata amani ya kudumu nchini Ukraine, lakini wiki iliyopita China ilitangaza kwamba haitashiriki. Akiwa mjini Beijing, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China, Mao Ning, amesema kuwa kuna tofauti kubwa kati ya muundo wa mkutano huo na matarajio ya China pamoja na matarajiojumla ya jumuiya ya kimataifa. Hata hivyo, Stoltenberg amesema hatua hiyo ya China sio ya kushangaza akieleza kuwa sio tu kwamba China ilishindwa kulaani uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, lakini pia Rais Xi Jinping na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, walitia saini makubaliano na kuahidiana ushirikiano usiokuwa na kikomo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW