1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Mkuu wa NATO aionya China dhidi ya kuisaidia Urusi kijeshi

5 Aprili 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg ametoa onyo kali kwa Beijing kutoipa Urusi silaha dhidi ya Ukraine.

Jens Stoltenberg
Katibu Muu wa Jumuiya ya Kujihami, NATO, Jens StoltenbergPicha: Kenzo Tribouillard/AFP

Stoltenberg amesema baada ya mkutano na mawaziri wa mambo ya kigeni wa Muungano huo kuwa utoaji wa msaada wa silaha za kivita wa China kwa Urusi utakuwa kosa kubwa la kihistoria lenye athari makubwa.

Washirika wa NATO waliwaalika wawakilishi kutoka Australia, New Zealand, Japan na Korea Kusini kuijadili China kufuatia ziara ya Rais wa China Xi Jinping mjini Moscow.

Pamoja na msimamo wa kiuchokozi wa Beijing kuelekea Taiwan, washirika wa NATO wamejadili athari za vita vya Ukraine kwa kanda ya Indo Pacific.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW