SiasaUkraine
Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg aizuru Ukraine
20 Aprili 2023Matangazo
Kama shirika la nchi 31 wanachama, NATO hutoa tu msaada usio wa silaha kwa serikali ya Ukraine kama vile jenereta, vifaa vya matibabu, mahema, sare za kijeshi na bidhaa nyingine. Stoltenberg alikuwa Kyiv kabla ya vita, lakini hii ndio ziara yake ya kwanza wakati huu wa vita na inasisitiza ahadi za muda mrefu za jumuiya hiyo katika ulinzi wa uhuru wa Ukraine.
Wakati huo huo, mkuu wa majeshi ya Ukraine amesema Urusi imefanya mashambulizi zaidi ya 20 ya ndege za rubani zisizoruka na rubani zilizotengenezwa Iran, katika saa 24 zilizopita. Amesema mifumo ya ulinzi ya Ukraine iliweza kuzidungua droni 21 kati ya 26 ambazo zimetengenezwa kuruka hadi sehemu inayolengwa na kisha kulipuka.