1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Joseph Borrell ashtushwa na mauaji ya mateka 6 wa Israel

1 Septemba 2024

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya,Joseph Borrell amesema ameshtushwa na mauaji ya mateka 6 raia wa Israel waliokuwa wakizuiliwa na kundi la wanamgambo la Hamas.

Miili ya watu hao ilikutwa katika mji wa Rafah katika ukanda wa Gaza.Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu katika Umoja wa Ulaya ameandika kupitia ukurasa wake wa X, kwamba watu hao wasiokuwa na hatia walipaswa kurudishwa kwa familia zao salama. Borrelle ametowa mwito wa kufikiwa usitishaji mapigano na kurudishwa kwa mateka waliobakia.

Familia za wanaoshikiliwa mateka zimetowa mwito wa kufanyika mgomo nchi nzima kuanzia leo Usiku kuishinikiza serikali kufikia makubaliano ya kuachiwa huru wanaoendelea kushikiliwa mateka katika Ukanda wa Gaza.

Mwito huo umekuja baada ya jeshi la Israel kupata miili ya watu sita waliokuwa mateka wa Hamas,katika njia za chini kwa chini kwenye mji wa Kusini mwa Gaza wa Rafah. Kuuliwa kwa watu hao kumeibuwa hasira miongoni mwa familia zao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW