1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Kiongozi wa Niger azungumza na Putin

27 Machi 2024

Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Niger Jenerali Abdourahamane Tchiani, Jumanne amezungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa njia ya simu kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kiusalama ili kukabiliana na vitisho vya sasa.

Niger | Jenerali Tchiani alipochukua madaraka baada ya mapinduzi dhidi ya Rais Bazoum
Jenerali Abdourahamane Tchiani, kiongozi wa kijeshi wa Niger amezungumza na Rais Vladimir Putin kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kiusalama Picha: ORTN/Télé Sahel/AFP/Getty Images

Taarifa hiyo imesema kuwa wakuu hao wawili pia walijadili miradi ya sekta mbali mbali na ushirikiano wa kimakakati wa kimataifa, bila ya kutoa maelezo zaidi.

Taarifa kutoka Ikulu ya Kremlin imeongeza kuwa viongozi hao wawili walielezea kuwa tayari kuanza mazungumzo ya kisiasa na ushirikiano wa manufaa kwa nchi hizo mbili.

Viongozi hao pia walizungumzia kuhusu hali katika maeneo ya Sahel na jangwa la Sahara huku msisitizo ukiwekwa katika uratibu wa mikakati ya kuhakikisha usalama na kukabiliana na ugaidi.

Jenerali Tiani, ambaye ameiongoza Niger tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Julai, alimshukuru Rais Putin kwa msaada wake nchini humo.