1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa shirika la IAEA atembelea kinu cha Nyulia cha Kursk

27 Agosti 2024

Mkuu wa Taasisi ya kimataifa ya kudhibiti matumizi ya nguvu za Atomiki, Rafael Grossi amewasili leo katika kinu cha Nyuklia cha Urusi cha Kursk.

Urusi| Kinu cha nyukilia |Kursk II
Kinu cha Nyuklia cha Urusi cha Kursk.Picha: Tatyana Simonenkova/TASS/IMAGO

Mkuu wa Taasisi ya kimataifa ya kudhibiti matumizi ya nguvu za Atomiki,Rafael Grossi amewasili leo katika kinu cha Nyuklia cha Urusi cha Kursk.Taarifa hiyo imeritiwa na shirika la habari la AFP ambalo limezungumza na msemaji wa shirika la Nyulia la Urusi Rosatam.

Mkuu wa IAEA Rafael Grossi  amesema anaongoza ujumbe kuelekea kwenyekinu hicho cha Nyukliakuendesha uchunguzi huru wa matukio yanayoshuhudiwa kufuatia mashambulizi ya kuvuka mpaka ya kushtukiza yanayofanywa na Ukraine katika eneo hilo la Kinu cha Nyuklia.

Ziara hiyo ya Grossi imekuja katika wakati ambapo imeripotiwa kwamba Urusi imeishambulia kwa siku ya pili mfululizo  Ukraine kwa silaha nzito nzito,usiku wa kuamkia leo. Takriban watu watano wameuwawa kufuatia mashambulizi hayo. Jeshi la Ukraine limesema kwa mara nyingine Urusi imerusha makombora ya masafa marefu ya aina mbali mbali dhidi ya miji kadhaa ya Ukraine.