1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa siasa kali za mrengo wa kulia afariki dunia Austria

Hamidou, Oumilkher11 Oktoba 2008

Jorg Haider aiaga dunia wiki chake baada ya ushindi katika uchaguzi wa bunge nchini Austria

KLAGENFURT:

Mkuu wa jimbo la Kärntner nchini Austria,mfuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia Jorg Haider amefariki dunia.Kwa mujibu wa polisi mwanasiasa huyo aliyekua na umri wa miaka 58 ameuwawa kufuatia ajali ya gari barabarani.Jorg Haider amejipatia umaarufu ndani na nje ya nchi yake kutokana na matamshi yake ya chuki dhidi ya wageni.Kifo chake kimejiri wiki mbili baada ya kurejea upya katika jukwaa la kisiasa nchini mwake.Katika uchaguzi wa bunge,mwisho mwa mwezi uliopita,chama chake cha "Bündnis Zukunft Österreich-au Muungano kwaajili ya mustakbal wa Austria" kilijikingia idadi kubwa ya kura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW