Mkuu wa Tume ya Ulaya ataka kuongeza uzalishaji wa silaha
30 Agosti 2024Matangazo
Von der Leyen amesema jukumu la kwanza la Ulaya ni kuilinda Ulaya. Ameongeza kuwa wakati Muungano wa Kijeshi wa NATO ukisalia kuwa kitovu cha nguvu jumuishi ya kiulinzi bado wanahitaji nguzo imara ya Ulaya.
Amesema hayo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa kimataifa wa usalama wa GLOBESEC, jijini Prague, Jamhuri ya Czech.
Soma pia:Mawaziri wa EU wajadili mafunzo ya wanajeshi wa Ukraine
Ameisistiza Ulaya kuwa macho, akisema itakuwa inajidanganya ikiwa itadhani kwamba imefanya vya kutosha kuhusiana na usalama, akionya nusu ya pilli ya muongo itakumbwa na kitisho zaidi.