1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa usalama Sudan ataka walokamatwa waachiliwe

Sekione Kitojo
30 Januari 2019

Mkuu wa usalama wa taifa nchini Sudan ameamuru kuachiliwa huru kwa wafungwa wote waliokamatwa katika maandamano ya  kupinga serikali.

Sudan Proteste gegen Präsident Al-Baschir
Picha: Reuters/M. N. Abdallah

Mkuu wa usalama wa taifa nchini Sudan ameamuru kuachiliwa huru kwa wafungwa wote waliokamatwa katika maandamano ya  kupinga serikali ambayo yameitikisa nchi hiyo kwa wiki kadhaa, hata  wakati  ambapo waandamanaji  wanapanga  kufanya  maandamano zaidi.

Amri hiyo iliyotolewa na Salah Ghosh imekuja huku kukiwa  na ukosoaji  mkubwa  kutoka  jumuiya  ya kimataifa kwa  kitengo  hicho  kufanya ukandamizaji mkubwa  kuzuwia  kusambaa kwa maandamano ambayo yalizuka kwanza mwezi Desemba.

Chama cha wataalamu nchini Sudan ambacho kinaongoza  kampeni ya  maandamano kimepuuzia  amri hiyo  ya  kuachiliwa  huru  watu  hao. Makundi  ya  haki  za binadamu  yanasema  kitengo  cha  usalama  wa  taifa NISS kimewakamata  watu 1,000, ikiwa  ni  pamoja  na waandamanaji, viongozi  wa  upinzani, wanaharakati  na waandishi  habari, kama  sehemu  ya  ukandamizaji  wa maandamano  hayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW