1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mkuu wa Wagner aonya juu ya Urusi kushindwa Bakhmut

6 Machi 2023

Kiongozi wa kampuni ya mamluki wa kijeshi ya Urusi, Wagner, Yevgeny Prigozhin ameionya Urusi kuwa itakuwa katika hali mbaya Bakhmut kutokana na ukosefu wa silaha.

Ukraine | Krieg | Videostill Wagner-Chef Jewgeni Prigoschin
Picha: Konkord Company Press Service/ITAR-TASS/IMAGO

Mkuu wa kampuni binafsi ya ulinzi nchini Urusi, Wagner yenye vikosi vya  mamluki vinavyopambana dhidi ya Ukraine, ametahadharisha kwamba Urusi iko katika nafasi mbaya kwenye eneo la mji wa mashariki mwa Ukraine wa Bakhmut kutokana na ukosefu wa silaha.

Taarifa hiyo ni ya hivi karibuni inayoonesha kuna mvutano kati ya serikali ya Kremlin na mkuu huyo wa Wagner, Yevgeny Prigozhin.

Maafisa wa Ukraine pia wameripoti kwamba viongozi wa brigedi ya Urusi inayopambana karibu na mji wa Vuhledar, kusini mwa Bakhmut wamekataa kutekeleza amri ya kushambulia baada ya kupoteza wanajeshi wake wengi kwenye mapambano ya kuuteka mji huo.

Hata hivyo, wizara ya ulinzi ya Urusi jana ilisema wanajeshi wake walishambulia kituo cha kijeshi cha Ukraine huko Zaporizhzhia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW