1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mkuu wa Wagner adaiwa kuwemo ndani ya ndege iliyoanguka

23 Agosti 2023

Watu 10 wamekufa baada ya ndege binafsi iliyokuwa ikitokea Moscow kwenda St. Petersburg kuanguka.

Russland Wagner-Gruppe Jewgeni Prigoschin
Picha: PMC Wagner/Telegram/REUTERS

Vyombo vya habari vya Urusi na maafisa wa anga wamesema kuwa mwanzilishi wa kundi binafsi la kijeshi la Urusi la Wagner, Yevgeny Prigozhin alikuwa kwenye orodha ya abiria wa ndege hiyo, lakini haikufahamika mara moja kama alikuwa ndani ya ndege hiyo.

Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinaeleza kuwa ndege hiyo ni mali ya Prigozhin, ambaye aliongoza uasi mwezi Juni dhidi ya jeshi la Urusi.

"Uchunguzi umeanzishwa kuhusu ajali hiyo ya ndege, ambayo imetokea usiku kwenye mji wa Tver. Kwa mujibu wa orodha ya abiria, miongoni mwa majina, limo la Yevgeny Prigozhin," imeleeza taarifa ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Urusi, Rosaviatsia.

Maafisa wa huduma za dharura wamesema miili minane imepatikana katika eneo la ajali.

Kumekuwa na maswali mengi mahali aliko Prigozhin tangu alipoongoza uasi huo, lakini hivi karibuni mkanda wa video ilimuonyesha kwenye mtandao wa kijamii wa Telegram akiwa barani Afrika. Hiyo ikiwa ni video yake ya kwanza tangu ulipofanyika uasi.

 

(DPA, AFP, AP)

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW