1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Golikipa wa Ujerumani Manuel Neuer atangaza kustaafu

30 Juni 2026

Golikipa mkongwe wa Ujerumani Manuel Neuer ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani mara tu baada ya kutolewa na Paraguay katika mchezo wa raundi ya 32 katika michuano ya Kombe la Dunia.

Manuel Neuer amekuwa kwa muda mrefu mlinzi wa lango la timu ya Ujerumani wa kutegemewa
Manuel Neuer amekuwa kwa muda mrefu mlinzi wa lango la timu ya Ujerumani wa kutegemewaPicha: Annegret Hilse/REUTERS

Golikipa mkongwe wa Ujerumani Manuel Neuer ametangaza kustaafu kuitumikia timu ya taifa ya Ujerumani mara tu baada ya kutolewa na Paraguay katika mchezo wa raundi ya 32 katika michuano ya Kombe la Dunia.

Alipoulizwa na waandishi wa shirika la habari la Ujerumani la ARD, Neuer amesema huo ndio ulikuwa mchezo wake wa mwisho akiwa na jezi ya timu ya taifa ya Ujerumani.

Hata hivyo, awali mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alishatangaza kustaafu kuichezea timu hiyo ya taifa kabla ya kurejeeshwa tena na kocha Julian Nagelsmann.kuondolewa mapema kwa Ujerumani: Tatizo ni nini?

Manuel Neuer alikuwa sehemu ya kikosi cha Ujerumani kilichobeba ubingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil na anamaliza muda wake akiwa na rekodi ya kipa aliyecheza mechi nyingi zaidi duniani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW