SiasaAsia
Mlipuko kwenye mgodi wa mawe nchini China wawauwa watu 90
23 Mei 2026
Matangazo
Shirika la habari la Xinhua limeripoti kuwa ajali hiyo katika mgodi wa Liushenyu ulioko katika jiji la Changzhi ilitokea jana jioni. Takriban wafanyikazi 247 walikuwa kazini wakati huo.
Xinhua pia imesema chanzo cha mlipuko huo bado kinachunguzwa na juhudi za uokoaji zinaendelezwa. Wengi wa wafanyakazi hao walijeruhiwa na gesi yenye sumu. Haya ni kulingana na shirika la habari la serikali CCTV.
Xinhua imeripoti kuwa Rais wa nchi hiyo Xi Jinping ametoa wito wa juhudi za kila namna kufanyika kuwaokoa waliotoweka na kufanywa kwa uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo huku akitaka waliohusika kuwajibishwa.
Mkoa wa Shanxi unajulikana kama mkoa mkuu wa uchimbaji madini wa makaa ya mawe nchini China.